(ABNA24.com) Utawala wa Kizayuni wa Israel umekerwa na hatua ya Rais Sebastián Piñera wa Chile akishirikiana na Idara ya Wakfu ya Kiislamu ya Quds na viongozi wa ngazi ya juu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kuzuru Msikiti wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu.
Kanali ya 12 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni imeakisi kukasirishwa utawala huo na ziara ya kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa Chile katika msikiti huo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Utawala wa Kizayuni imelazimika kumuita balozi wa Chile na kumtaka atoe maelezo kuhusiana na kadhia hiyo. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa sheria na maazimio ya kimataifa, msikiti wa Al-Aqsa ni kati ya maeneo matukufu ya Kiislamu ya taifa la Palestina. Aidha msikiti huo kama nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu kwa taifa la Palestina pamoja na mji wa Quds unakopatikana msikiti huo, vimekuwa vikilengwa na hatua haribifu za utawala katili wa Kizayuni.
Hatua hizo haribifu za utawala wa Kizayuni zina lengo la kuangamiza kabisa utambulisho wa Kiislamu wa mji wa Quds na badala yake kusimika alama na nembo za Kizayuni katika eneo hilo la Kiislamu. Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Sebastián Piñera wa Chile kuonyesha uungaji mkono wake kwa Palestina. Mwishoni mwa mwaka jana pia rais huyo alikutana na Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina huko Santiago, mji mkuu wa Chile ambapo aliweka wazi msimamo wa nchi yake wa kuiunga mkono Palestina na kusisitiza kuwa, kuna haja ya kupewa uhuru taifa la Palestina.
/129
1 Julai 2019 - 02:57
Msimbo wa Habari: 956473
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekerwa na hatua ya Rais Sebastián Piñera wa Chile akishirikiana na Idara ya Wakfu ya Kiislamu ya Quds na viongozi wa ngazi ya juu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kuzuru Msikiti wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu.